JINSI JANJAJANJA INAVYOTIBUA MAHUSIANO YA KIMAPENZI

black-couple00

Wengine huwa ni tabia yao ya asili, siyo mkweli kuanzia malezi ya wazazi wake kwani hayasisitizi juu ya ukweli. Ameshazoea kufanya mambo kiujanja ujanja! Kwa mpenzi wa aina hii ni vigumu sana kudumu naye. 

Ni mwepesi wa kutamka maneno ya mapenzi lakini ndani ya moyo wake kuna vitu viwili, kwanza anakutamani wewe na pesa zako na wakati huohuo anatamani kuwa na bwana mwingine kwa ajili ya kuongeza kitega uchumi, hili ni tatizo.

Mwanamke wa aina hii siyo vigumu kukuita majina mazuri ya kimapenzi lakini akiwa hamaanishi kutoka moyoni mwake kwamba anakupenda, Hawa wapo wengi lakini ni vigumu sana kuwagundua mapema, Hawa huharibu kabisa maana halisi ya mapenzi. 

black-couple

Ngoja nikuulize wewe unayemsaliti mpenzi wako, unavyomfanyia mwenzako hivyo unadhani yeye hana moyo? Hivi hujui kuwa mwenzako anakupenda kwa mapenzi yake yote na amekuchagua wewe uwe mwandani wake? Siku akijiua kwa sababu yako utakuwa katika hali gani? Hebu acha utapeli wako wa mapenzi haraka sana.

Kuwa muwazi na kama unadhani haupo tayari kuwa na mpenzi basi mwache huru atafute mwingine mwenye msimamo uendelee na mambo yako na kama ni kujiuza ujiuze vizuri lakini ukijua kuwa siku moja utakuja kuingia mahali pabaya. Achana na tamaa za muda mfupi ambazo mwisho wake ni mbaya.

Huyo mwanaume anayekudanganya leo, ujue kabisa kesho hayupo na wewe na atakuwa amekuachia virusi vyako vya kutosha, Kama umeamua kujitoa sadaka ni bora ukafa peke yako kuliko kumwangamiza na mwenzako ambaye hana hatia zaidi ya penzi lake la dhati kwako.

Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!