Posts

Showing posts from April, 2016

Msajili wa Vyama Avikaba Koo Vyama 21 Vya Siasa Ambavyo Havijakaguliwa......Kwa Mujibu wa CAG, ni Chama cha CUF Pekee ndo Kimekaguliwa

Image
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametoa miezi mitatu kwa vyama 21 ambavyo havijakaguliwa kuwasilisha hesabu zake. Kauli ya Jaji Mutungi imekuja siku nne baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad kutoa taarifa juu ya ukaguzi wa hesabu katika vyama vya siasa 22 vyenye usajili wa kudumu, CAG alieleza kati ya vyama hivyo, chama cha CUF pekee ndicho kilikuwa kimepeleka hesabu zake kwa kipindi cha miezi sita, kati ya Januari hadi Juni 2015. Alisema vyama vingine 21 havikuwasilisha vitabu vya hesabu kwa ajili ya ukaguzi kinyume na kifungu cha 14 cha Sheria ya vya ma vya siasa namba 5 ya mwaka 1992. Akizungumza jana nje ya viwanja vya Bunge, Jaji Mutungi alisema ukaguzi wa fedha katika vyama ni suala la kisheria na lina mchakato wake, akisisitiza kuwa ofisi yake imeisoma taarifa ya CAG na inaifanyia kazi kwa kuvipa vyama hivyo miezi mitatu. “Kwa mujibu wa sheria tunatakiwa kuvikumbusha vyama kufanya ukaguz

Wabunge MABUBU Kubanwa Bungeni......Ni Wale Wanaoshiriki Vikao vya Bunge Lakini Hawachangii Chochote

Image
Kiti cha Spika wa Bunge kimesema ipo haja ya kufanya marekebisho ya Sheria pamoja na Kanuni ili kila mbunge apate posho kulingana na kazi aliyofanya bungeni, badala ya utaratibu wa sasa wa kuangalia mahudhurio pekee.  Aidha, kimewataka wabunge kubadilika na kuacha tabia ya kuchukua posho za vikao vya Bunge bila kuzitolea jasho. Kauli hiyo imekuja kutokana na Mwongozo ulioombwa Aprili 25, mwaka huu na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) ambaye alikitaka kiti cha Spika kutoa Mwongozo kuhusu usahihi wa wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kulipwa posho na mishahara wakati hawashiriki na kutimiza wajibu wao wa kuchangia kwenye mjadala wa Bunge la Bajeti linaloendelea katika Mkutano wa Tatu wa Bunge la 11. Bashe alisema mbunge huyo alitumia Kanuni ya 68(7) ya Kanuni za Kudumu za Bunge akiomba Mwongozo wa Spika kutokana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuamua kutoshiriki mjadala unaoendelea bungeni, lakini wabunge hao wanasaini na kulipwa mishahara na posho.

Watakaolipa mishahara HEWA kuburuzwa Mahakamani

Image
Serikali imesema vigogo wa juu katika utumishi wa umma, watakaobainika kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha ulipaji wa mishahara hewa, watafunguliwa kesi ya jinai. Aidha, imesema ifikapo Julai mosi, mwaka huu Halmashauri zote nchini ziwe zimefunga na kutumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato yake ya ndani na zimetakiwa kusitisha ukusanyaji kwa njia ya mawakala. Katika hatua nyingine imesema hadi kufikia Machi, 2016, watumishi 90 wamechukuliwa hatua mbalimbali za kinidhamu na wengine kufikishwa mahakamani kwa kukiuka taratibu na sheria za kazi wakiwemo wakurugenzi watendaji (DED) wa halmashauri watano ambao wamevuliwa madaraka. Hayo yalisemwa kwa wakati tofauti na mawaziri wawili katika Ofisi ya Rais, walipowasilisha hotuba za bajeti kwa ofisi zao kwa mwaka ujao wa fedha bungeni mjini Dodoma jana.  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki akiwasilisha hotuba ya ofisi hiyo, alisema kuanzia sasa kiongozi wa s

Sakata la UDA Laitikisa Serikali

Image
Wakati Serikali ikiendelea kuchunguza mikataba kati ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda) na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Dart) kuhusu Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ametia pilipili kidonda kwa kuibua udanganyifu unaolizunguka shirika hilo. Kwenye ripoti yake ya mwaka wa fedha 2014/2015 aliyoitoa bungeni Jumatatu, CAG Profesa Mussa Assad amebainisha kwamba Dart ilifanya makubaliano na msimamizi wa uendeshaji, Uda-RT kutoa huduma ya mpito ya usafiri kwa kutumia mabasi 76 yenye vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Tofauti na makubaliano hayo, Uda ilinunua mabasi 140 ambayo yalikuwa na nembo ya Uda-RT badala ya Dart kinyume na vigezo vilivyoainishwa kwenye mkataba. Meneja wa Miundombinu wa Dart, Mhandisi Mohamed Kuganda alisema wenye taarifa sahihi ni Uda-RT. Hata hivyo, alikiri kufahamu ununuzi wa mabasi hayo na kusema waliwauliza Uda-RT na wakajibiwa kuwa, “barabara za kutumika mabasi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya April 28

Image

CHELSEA WABINGWA TENA KOMBE LA FA LA VIJANA ENGLAND

Image
Dujon Sterling akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ya Chelsea bao la kwanza katika ushindi wa 3-1 kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la England kwa vijana wa umri huo dhidi ya Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge, London. Mabao mengine ya Chelsea yalifungwa na Tammy Abraham na Fikayo Tomori huku bao pekee la Man City likifungwa na Brahim Abdelkader Diaz, hivyo makinda hayo ya The Blues kutwaa tena ubingwa wa U-18 wa FA kwa ushindi wa jumla wa 4-2 baada ya awali kutoa sare ya 1-1 mjini Manchester.

UCHUKUZI SC, TAMISEMI KAMA FAINALI KESHO

Image
Nahodha wa timu ya Uchukuzi SC, Godwin Ponda akimtambulisha mgeni rasmi wa mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tamisemi, Kaimu Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Mei Mosi, Joyce Benjamin kwa kipa wake Herbat Steven, nyuma ni mkuu wa benchi, Kenneth Mwaisabula. Uchukuzi walifungwa magoli 2-0. Mwamuzi Robert Mkatakiu (aliyeshika kadi ya njano) akimuangalia mchezaji Kombo Ally wa Tamisemi aliyelala chini baada ya kuumia. Mchezaji huyo alionyeshwa kadi hiyo pamoja na nahodha wa Uchukuzi Godwin Ponda (kulia). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0. Wachezaji wa timu za Uchukuzi SC na Tamisemi wakisubiri mpira wa kona upigwe na Omary Said wa Uchukuzi (haonekani pichani). Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0. Kipa wa Tamisemi,, Leonard Mkinga (katikati ya goli) akiwapanga wachezaji wake kabla Uchukuzi hawajapiga mpira wa kona. Tamisemi walishinda kwa magoli 2-0. Tatu Kitula (mwenye mpira) wa Uchukuzi SC akijiandaa kufunga bao katika mchezo wa netiboli wa mashindano ya Mei Mosi dhidi ya TPDC. Uch

BOSTON CITY CAMPUS TANZANIA, BRANCH NOW OPEN

Image
Boston City Campus and Business College carries a legacy of over 20 years in South Africa. It currently has 44 branches with over 25000 students studying every year. In Tanzania, Boston has opened its first branch outside South Africa, 45 th Branchin total this year.   Boston offers Professional Courses and Short Learning Programs with plans to introduce tertiary education in the future. These are further learning programs which will enhance one’s skills and assist to get better jobs. They have extended their wide range of courses which they offer in South Africa in various fields to Tanzania.    Students can choose from multiple course under various categories such as Accounting, ICT, Business Management, Business Communications, Marketing and many more. There are professional courses offered at their college such as ACCA and CompTIA certified A+, N+ and many more.   The teaching methodology Boston is bringing to Tanzania is quite different from the conventional way of