Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo,Freeman Mbowe ametangaza kusitishwa kwa maandamano ya Oparesheni UKUTAyaliyokuwa yamepangwa kufanyika kesho nchi nzima hadi tarehe moja Octoba. Akizungumza na wanahabari leo, makao makuu ya chama hicho, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mbowe amesema, Chadema inalazimika kuahirisha maandamano na mikutano ya kesho kutokana na kuheshimu wito wa viongozi wa dini zote waliowaomba. “Viongozi wa dini zote hapa nchini kuanzia, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania, Rais wa Baraza la Maaskofu (TEC), Katibu Mkuu wa Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT),Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Mufti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) na Mufti Mkuu wa Zanzibar, wametusihi tuahirishe ili wao wazungumze na Rais John Magufuli kutafutia suluhu suala hili,” amesema Mbowe. Mbowe amezitaja taasisi na watu ...