Mfalme Mohammed VI, ambaye alishiriki kikao cha Umoja wa Afrika Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, alifanya ziara nyingi za kikazi katika miji mikuu ya nchi za Afrika ili kupata uungwaji mkono. REUTERS/Maghreb Agence Press/Pool Viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika wamemua Jumatatu wiki hii kuikubalia Morocco kujiunga upya na Umoja wa Afrika. Wakati huo huo Tume ya Umoja wa Afrika imempata kiongozi mpya, huku rais wa Guinea, Alpha Condé, alkichaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Afrika Angalau Marais na viongozi wa serikali 39 kati ya 54 wanachama wa Umoja wa afrika wamepiga kura ya ndio kwa Morocco kujiunga upya na AU, kwa mujibu wa rais wa Senegal Macky Sall, ambaye ameshiriki katika zoezi la kuchunguza faili ya Morocco Jumatatu wiki hii mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia. Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amethibitisha kuwa "nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Afrika walibaliwa ombi la Morocco kurejea katika Umoja wa Afrika." Mwaka 1984, Morocco...