Serikali, imesema watumishi wa umma walioorodheshwa kwenye orodha ya watumishi wa umma wenye vyeti feki, wakati hawakutakiwa kuwekwa, wakate rufaa. Kauli hiyo, ilitolewa jana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. “Kama mtakumbuka, uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma, ulihusisha vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita, ualimu na taaluma zingine. “Baada ya uhakiki huo, iliagizwa watumishi 9,932 waliokuwa na vyeti feki, waondolewe katika ajira, watumishi 1,538 wenye vyeti vyenye utata kwa maana kwamba vinatumiwa na watu zaidi ya mmoja, wathibitishe vyeti vyao kabla ya Mei 15 mwaka huu na mishahara yao isimamishwe hadi uhakiki utakapokamilika. “Wale watumishi 11,596 waliogundulika kuwa na vyeti pungufu, wanatakiwa kuwasilisha vyeti vyao vikaguliwe kabla ya Mei 15, mwaka huu, vinginevyo watachukuliwa hatua. “Lakini, wale wanaodai kwamba wamewekw...