Posts

Showing posts from September, 2017

BURUNDI YAPOKEA AWAMU YA KWANZA YA WAKIMBIZI KUTOKA TANZANIA

Image
Burundi imepokea wakimbizi 301 wanaorudi kutoka Tanzania, ikiwa ni sehemu moja ya wakimbizi elfu 12 wanaotarajiwa kurudi Burundi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Wakimbizi hao wote wanaotoka kambi ya Nduta mkoani Kigoma, walivuka mpaka kwa msaada wa shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR, chini ya mchakato wa kuwarudisha kwa hiari utakaomalizika tarehe 31 Desemba, mwaka huu.   Baada ya kuwapokea wakimbizi hao, msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Bw Terence Ntahiraja ameishukuru Tanzania kwa kuwapokea warundi wanaotafuta hifadhi.

HUSSEIN BASHE ANENA KUHUSU HALI YA USALAMA...ADAI HAKUNA ALIYE NA UHAKIKA NA MAISHA YAKE

Image
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amefunguka na kuomba muongozo wa Spika kuhusu hali ya usalama wa nchi, kwa kuwa matukio ambayo yanaendelea kutokea ya kihalifu hayana hitimisho lake. Bashe amesema hayo wakati akiomba muongozo ndani ya bunge kwa kumtaka Spika wa bunge Job Ndugai kukubali ombi la kamati ya usalama ya bunge likutane na vyombo vya usalama ili yaweze kupatikana majibu ya matukio yanayoendelea kutokea. " Mhe. Spika katika taifa letu katika kipindi cha muda mrefu kumekuwa yakitokea matukio mbalimbali ambayo sisi kama wawakilishi wa wananchi tuna wajibu wa kupata taarifa sahihi juu ya muendelezo wa matukio hayo ambayo hayana hitimisho" , amesema Bashe. Pamoja na hayo, Bashe aliendelea kwa kusema  "sisi tunawawakilisha Watanzania milioni 50 lakini matukio haya yanayotokea yanaharibu heshima ya taifa letu ningekuomba kama utaridhia na wabunge wataniunga mkono, uitake kamati yako ya ulinzi na usalama ya bunge tukufu ikutane na vyombo vya ulinzi na usalama ili