Posts

CCM Yatoa Tamko Baada ya Wabunge Wake Kufikishwa Mahakamani Leo Kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Kwa kipindi cha hivi karibunin kumekuwepo na tuhuma za baadhi ya wabunge kujihusisha na masuala ya rushwa. Tuhuma hizo zimekuwa zikifanyiwa kazi na vyombo vya dola na kwamba tayari baadhi ya wabunge wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma hizo. Chama cha Mapinduzi (CCM) kinasikitishwa sana na tuhuma hizo, hasa pale zinapowahusisha wabunge ambao ni wawakilishi wa wananchi  na kinaunga mkono jitihada za vyombo vya dola katika kutafuta ukweli wa tuhuma hizo. Lazima ifahamike kuwa vitendo vya rushwa havina itikadi,dini, wala kabila na kwamba havikubaliki kwa namna yoyote kwani vina madhara makubwa kwa taifa. CCM inavishauri vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua stahiki wabunge wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa. Chama cha mapinduzi kwa upande wake hakitasita kuwachukulia hatua kali za kinidhamu wabunge wake watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.  

TCRA WAIKABIDHI LESENI YA BIASHARA KAMPUNI YA AGANO SAFI

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services).  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo Ya Nangolo leseni ya biashara itakayoiwezesha kutoa huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya huduma anuai kwa njia ya kidigitali’ (Digital Payment Services). Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Huduma za Kisheria wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fortunata Mdachi pamoja na Amos Shiyuka (kushoto) wakishuhudia. MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeikabidhi leseni ya biashara kampuni ya Agano Safi inayokuja kuwekeza katika huduma za mfumo wa malipo mbalimbali kwa kutumia mtandao ‘malipo ya hu...

Breaking News: Wabunge Watatu Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Rushwa

Image
Pichani kutoka kushoto ni Mbunge wa Mwibala,Mh.Kangi Lugola,Mbunge wa Mvomero Mh.Sadiq Murad pamoja na Mbunge wa jimbo la Lupa Mh.Victor Mwambalaswa ** Wabunge watatu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wamefikishwa mahakama ya Kisutu leo kwa tuhuma za rushwa. Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati za kudumu za Bunge wanatuhumiwa kushawishi na kupokea rushwa  ya shilingi Milioni 30 toka kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Gairo  Mwendesha Mashitaka wa Tume ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mahela Ndimbo mbele Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu,  Thomas Simba amesema tukio hilo lilitokea  Machi 15 mwaka huu  majira saa 2  had saa 4 katika hoteli ya Golden Tulip jijini Dar es Salaam. Ndimbo alidai mahakamani hapo kuwa washitakiwa hao wakiwa wajumbe Kamati Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) waliomba  rushwa ya sh.milioni 30 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Gairo, Mbwana  Magota. Hakimu Mkaz...

Vodacom yadhamini michezo shule ya sekondari Nganza

Image
  Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akigawa Fulana za Vodacom kwa wanafunzi wa Nganza Sekondari katika Tamasha la michezo la shule hiyo waalilolidhamini jijini Mwanza jana.    Kanda: Mkuu wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom. Picha na Lordrick Ngowi    Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishndana kukimbia na magunia jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom.   Halima Juma na Jesca Balakekenwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula keki na soda jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom.    Muntancy Rashidi na Rosemery Yohana wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nganza ya jijini Mwanza wakishindana kula chakula jana katika tamasha la michezo lililodhaminiwa na Vodacom   Mwanafu...

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI TB III

Image
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA Kamati  ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeipongezaSerikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kwa kujenga jengo zuri la tatu la abiria (TB III)  litakaloboresha zaidi huduma za usafiri wa anga. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Norman Sigalla (Makete) wakati Wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea jengo hilo katika ziara yao ya kukagua miradi ya Serikali mwanzoni mwa wiki. Jengo hilo linajengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kwa Euro milioni 254 (sh. Bilioni 560) za mkopo kutoka Benki ya HSBC ya Uingereza na CRDB kwa dhamana ya Serikali ya Tanzania na Uholanzi. Tayari TAA imeshamlipa Mkandarasi wake, Bam International ya Uholanzi, Euro milioni 96 baada ya kukamilisha asilimia 60 ya kazi. Jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kw...

TRA Yakamata Magari Matano ya TFF Kutokana na Malimbikizo ya Kodi ya Bilioni 1.118

Image
Mamlaka ya mapato nchini (TRA) imeibukia tena Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lakini safari hii haijapiga kufuli account za TFF badala yake imeondoka na magari matano yanayomilikiwa na shirikisho hilo kutokana na kulidai kiasi kikubwa cha kodi. TRA imeamua kuchukua magari hayo ikitaka TFF kulipa deni la malimbikizo ya kodi mbalimbali wanayodaiwa ili warejeshewe magari yao. Richard Kayombo ni afisa wa TRA amethibitisha kuyakamata magari hayo yanayomilikiwa na TFF lakini amefafanua sababu zilizopelekea kufanya hivyo. “Ni kweli tumekamata magari matano ya TFF na hayo magari yamekamatwa kama sehemu ya mwendelezo wa kuweza kupata mapato yanayotokana na deni la kodi ambalo TFF hawajalipa. “Mpaka sasa tunawadai billion 1.118 ambayo ni kodi mchanganyiko kuanzia mwaka 2010 hadi 2015. Ikumbukwe hapo nyuma tulikamata account zao kwasababu deni lilikuwa ni billion 1.6 na tukaweza kupunguza sehemu ya deni lakini bado halijaisha na ndiyo sababu ya kukamata hayo magar...

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii yatembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya TBC-Kisarawe.

Image
  Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya jamii wakipitia taarifa ya shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe pwani na maendeleo yake. Mkurugenzi wa shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw.Ayoub Ryoba akiwasilisha  taarifa ya shirika hilo  kwa wajumbe wa wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kuhusiana na upanuzi wa masafa ya usikivu kisarawe Pwani.Wengine pichani ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye,Naibu Waziri wa wizara hiyo Bi.Anastazia Wambura na mwenyekiti wa kamati hiyo Bw.Peter Serukamba.Picha na Daudi Manongi-Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye (wa pili kulia) akiwasilisha jambo kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii walipotembelea mradi wa upanuzi wa masafa ya usikivu ya shirika la utangazaji...