Posts

GAZET LA MTANZANIA LA ZINDUA MWEONEKA MPYA “MTANZANIA LIMEBORESHWA.

Image
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)Ltd, Absalom Kibanda, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”.Kulia ni Mhariri Mtendaji wa  Mtanzania, Dennis Msacky na Meneja Masoko wa kampuni hiyo. Mhariri wa Gazeti la Mtanzania, Dennis Msacky.akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana. kuhusu uzinduzi wa mwonekano mpya wa Gazeti la Mtanzania lenye kauli mbiu ya “Mtanzania Limeboreshwa”Katikati ni Mhariri Mtendaji Kampuni ya New Habari(2006)Ltd, Absalom Kibanda na Meneja Masoko wa Kampuni hiyo, Michael Bugidira. Picha na Mpiga Picha Wetu  (P.T)

TAZAMA Nyumba Aliyokuwa Anaishi Mtangazaji Millard Ayo Kabla Mambo Hayajamyookea..!!

Image
TBT mtu wako wa nguvu nikiwa nje ya chumba nilichokua naishi kwa miaka mitatu 2005-2008 Keko Machungwa Dar es salaam toka wakati naanza kazi ya Utangazaji/Uandishi kwenye Radio na Gazeti la #MsemaKWELI Hakijawahi kuwa na umeme kwa miaka yote, pamoja na yote sikuwa na neno kuishi hapa... jirani yangu alikua Bwana @yonathanlanda ndio mambo ya kupasi, kuchaji simu na kuangalia TV nilikua nilimalizana nayo kwake, tusikate tamaa watu wangu, kama una nia... hapo ulipo unapita tu.

Benki Zaanza Kuwakamua Watanzania kwa Kuongeza kodi (VAT) ya 18%

Image
Ukifanya muamala wowote wa kutoa pesa benki kuna makato mfano kwa CRDB ni 2,200. Maana ya hii kodi ni kuwa sasa utakatwa TZS 2,596. Vile vile ukifanya malipo kwa njia ya TISS makato yalikuwa ni TZS 10,000; kwa sasa utakatwa TZS 11,800. TULIPE KODI KWA MAENDELEO YA NCHI YETU

Jerry Muro Aitwa Kamati ya Maadili TFF....Kisa Hichi Hapa

Image
MKUU wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanha Jerry Muro ameitwa kwenye kikao cha kamati ya maadili cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF kufuatia kitendo chake cha kupingana na kuishambulia katika kuelekea mechi yao ya Kimataifa ya kombe la Shirikisho Barani Afrika uliofanyika Juni 28.  Hiyo inakuwa ni mara ya tatu kwa Muro kuitwa na anatakiwa kufika Julai 02 katika ofisi za TFF saa Nne asubuhi au kama atashindwa kufika basi atume mwakilishi wake au utetezi wake kwa njia ya maandishi. Muro amethibitisha hilo na kusema kuwa amepokea barua hiyo na hii ikiwa ni mara ya tatu na katika mara zote amekuwa anashinda kwa hoja na kwa.wakati huu mkakati wao mkubwa kuona nafungiwa kujihusisha na masuala ya mpira na zaidi anashangaa ni jinsi gani wanasema amewashambulia kupitia vyombo vya habari. Barua hiyo inamtaka Muro kujitokeza siku hiyo au hata kama hatoweza kufika basi atume utetezi wake kwa maandishi au mwakilishi wake na hata kama hatofika basi kikao cha kamati ya maadili ...

MAHAKAMA KUU KANDA YA DAR ES SALAAM YASHIRIKI MAONESHO YA SABASABA

Image
Mtendaji Mkuu wa Mahakama  Tanzania Bw. Hussein Kattanga akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtendaji Mkuu Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Bi. Mary Shirima wakati wa maonyesho ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijin Dar es Salaam Wanausalama wakiimarisha ulinzi katika viwanja vya sabasaba ili wafanyabiashara na wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa amani. Mwanafunzi kutoka chuo cha VETA wa pili kutoka kulia akiwaelekeza baadhi ya wananchi ubunifu wa kutengeneza boti itakayokuwa inatembea barabarani kwa kuendeshwa na dereva mpaka baharini Picha na Benjamin Sawe  (P.T)

Waziri Mkuu Awataka Wanufaika wa Mikopo ya Elimu Juu Kurejesha mikopo waliyopewa.

Image
Wanufaika wa Mikopo ya Elimu ya Juu ambao tayari wapo katika ajira wametakiwa kurejesha marejesho ya mikopo waliyopewa kutokana na mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kutegemea fedha hizo kuendelea kuwakopesha wanafunzi wengine. Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akiwasilisha hotuba ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la kumi na moja. “Uwezo wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu kuwahudumia walengwa unajengwa na fedha zinazotengwa kila mwaka katika mipango na Bajeti pamoja na marejesho ya mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika,” alisisitiza Mhe. Majaliwa. Aliendelea  kusema kuwa Serikali inaendelea kufanya maboresho ya kimfumo na kisheria ili kuimarisha urejeshwaji wa mikopo.  Aidha amewaagiza waajiri wote Nchini kutekeleza wajibu wao wa kuingiza makato ya marejesho wa mikopo ya wanufaika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa baada ya kuwasiliana na Bodi ya Mikopo. Vile vile Mhe. Majaliwa amese...

TP Mazembe Jeuri, Kumsajili Mchezaji Huyu wa Yanga Kwa Gharama Yoyote

Image
Moja ya kauli zilizotolewa na TP Mazembe walivyotua Tanzania kupambana na Yanga, ni kuwea mbali na mechi hiyo pia walipanga kuondoka na wachezaji wenye vipaji kutoka Tanzania kama walivyofanya kwa Mbwana Samatta. Na baada ya mechi hiyo ya juzi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0, jina la winga mpyawa Yanga, Juma Mahadhi, ndio lilinasa kwenye akili za mashabiki na mabosi wa Mazembe kama ilivyokuwa kwa Samatta mwaka 2011. Kwa sababu uwezo alioonyesha juzi na Mahadhi ambaye alikua anacheza mechi yake ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga, umewashawishi mashabiki na viongozi wa mazembekubeba jina la kinda huyo na kupania kulipeleka kwa tajiri wa klabu hiyo, Moise Katumbi. Inafahamika kuwa  Katumbi anawakubali na kuwaamini sana sana mashabiki wake na siku zote wakimpa jina la mchezaji huwa tayari  kuvunja benki kumsajili kama alivyofanya kwa Samattamiaka mitano iliyopita. Katika mchezo wa juzi licha ya ugeni wake katika mechi kubwa za kimat...