Lipumba Aendelea Kung'ang'ania Uenyekiti Wake CUF
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Prof Lipumba ameendelea Kung’ang’ania kiti cha uenyekiti wa chama chake cha CUF na kusema kikao kilichokaa jana visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya. “Kikao hicho hakikuwa halali, haiwezekani Baraza Kuu linakaa halafu Naibu Katibu Mkuu Bara hajui, wala hakujulishwa, na bado kuna wajumbe wengine hawakuhusishwa” Alisema Prof Lipumba Lipumba aliongeza kuwa ni kweli alijiuzulu uenyekiti, lakini baadaye aliamua kuandika barua kwa Katibu Mkuu ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu na sasa yeye ndiye Mwenyekiti halali wa chama hicho. “Nilimuandikia barua ya kurudi kwenye nafasi yangu, akasema anasubiri ushauri wa kisheria, lakini hadi sasa hakuna kitu, hiyo inamaanisha kuwa sasa mimi naendelea na nafasi yangu, na niko ngangari kama mwenyekiti” Alisema Prof Lipumba. ...