Posts

HALMASHAURI ZOTE NCHINI ZAAGIZWA KUWASILISHA TAARIFA ZA MAENDELEO YA MPANGO WA BIASHARA NCHINI

Image
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.   Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti wa Kamati...

FAMILIA YASUSIA MAITI MKOANI GEITA YATAKA MARIDHIANO NA JESHI LA POLISI.

Image
Baaadhi ya ndugu wa marehemu wakiwa wameketi kwa masikitiko wakisubilia muafaka wa kuzikwa kwa ndugu yao. Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo akikiri kutokea kwa tukio hilo mbele ya waandishi wa habari. wanafamilia wakiwa kwenye masikitiko. Famili ya mzee Isaya Neligwa wa Mto wa Mbu Mkoani Arusha  imesusia kuchukua maiti ya Jeremia Isaya ambayo imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita ,huku wakidai kupata maridhiano na jeshi la polisi kwani ajali hiyo ilisababishwa na  gari ya polisi yenye nambari za usajili PT 4026 iliyomgonga na kusababisha  kifo chake.   Tukio hilo la ajali lilitokea tarehe 12 mwezi wa pili majira ya saa 12:30 jioni  Kwenye eneo la Mwatulole kata ya Buhalahala ambapo gari la kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) likitokea Kasamwa kuja mjini Geita lilimgonga kijana huyo wakati alipokuwa akivuka barabara kwanda upande mwingine.   Moja kati ya wanafamilia ,Bw Elineema Mafi...

MKUU WA SHULE MKOANI SINGIDA AJINYONGA HADI KUFA

Image
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake. Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo. Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe. “Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina...

WAZIRI NAPE MGENI RASIMI FAINALI ZA ULEGA CUP ZITAKAZOFANYIKA MACHI 5 MKURANGA

Image
Timu ya kata ya Tengelea, Tengelea FC  imefunzu kuingia katika fainali ya Ulega Cap baada ya kuifunga Timu ya Mwandege FC  bao 1 – 0 katika mcheezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana . Bao la timu ya Tengelea lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia mchezaji  wao Andew Joseph aliyepokea cross ambayo ndio ilipa ushindi timu hiyo. Timu ya kata ya Tengelea, itaingia fainali kwa kukipiga na timu ya Kisiju na mechi itanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Mwandege FC na Lukanga FC. Mgeni rasmi katika fainali za Ulega CUP ni Waziri Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye. Akizungumza na waandishi wa habari muandaji wa mashindano hayo Mbunge wa  Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa mashindano yameibua vipaji ya vipya. Amesema kuwa inahitaji uwekezaji katika michezo kutokana na vijana kuonyesha vipaji vyao ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.  Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wacheza...

TAZAMA PICHA:ALLY KIBA APOKEWA KISHUJAA, NI BAADA YA KURUDI NA TUZO YA MSANII BORA WA KIUME AFRIKA

Image
 Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika Ally Kiba akiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere  akitokea nchini Afrika Kusini mara baada ya kukabidhiwa tunzo yake ya MTV kama msanii bora wa kiume Afrika                  Mashabiki wa AlyKiba ambao walifika katika uwanja wa ndege wa JNA jijini Dar es Salaam wakiwa na mabango kama wanavyoenekana pichani  Kiba kielekea kwenye gari maalum aliyoandaliwa mara baada ya kuzngumza na mashabiki wake  Aly Kiba akiwa na Meneja wake  Seven Mosha mara baa da ya kuingia katika gari hiyo maaalum  Ally Kiba akiwa katika mitaa ya Kariakoo huku akiwa amezunguskwa na mashabiki mbalimbali ambao walipata fursa ya kuona Tunzo yake ya Mtv base kama msanii bora wa kiume Afrika  Mashab...

TFDA YATOA TAHADHARI KUHUSIANA NA DAWA AINA YA P-500(PARACETAMOL)

Image

HASHIMU RUNGWE AMJULIA HALI GODBLES LEMA

Image
Mwenyekiti  wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe, amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), ambaye   bado yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo mkoani Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Arusha jana baada ya kuonana na mbunge huyo, Rungwe alisema baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye jamii yanasababishwa na baadhi ya watawala. Alisema hali hiyo imekuwa ikiibua chuki miongoni mwa wananchi   jambo ambalo si zuri na linahitaji kukemewa. Kiongozi huyo alimtembelea Lema    akiwa  amefuatana  na viongozi mbalimbali akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Chauma, Kayumbo Kabutali  na wabunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na Moshi Vijijini, Antony Komu,  wote wa Chadema “Historia ya zamani inatufunza matatizo yanayotokea katika jamii yanachangiwa na mambo yanayotendwa na baadhi ya watawala  ambayo yanaleta chuki. “Na chuki siyo kitu kizuri kwa sababu inazidi k...