Posts

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 18

Image

Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia

Image
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku). Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua. Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana  saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.

TANESCO yakanusha taarifa ya kuuza mitambo ya Kinyerezi

Image
Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),limekanusha taarifa ya gazeti la Mwananchi iliyosema kuwa vifaa vya mitambo ya Kinyerezi hatarini kwa kuuzwa. Tanesco imekanusha taarifa hizo, kuwa si za kweli ni upotoshaji kwa umma huku shirika hilo likidai linaendele na ulipaji kodi. Advertisement ==

TAKUKURU yaisaidia Serikali kuokoa Sh53 bilioni

Image
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kuokoa Sh bilioni 53.9 kutokana na uchunguzi na operesheni mbalimbali zilizofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika mwaka 2016/2017. Amesema kiasi hicho cha fedha ni kikubwa mno, ikilinganishwa ni Sh bilioni 7 tu zilizookolewa katika mwaka 2015/2016. Alisema hayo jana wakati akifungua semina ya Mtandao wa Wabunge wa Afrika walio katika Mapambano ya Rushwa (APNAC) Tawi la Tanzania kwenye ukumbi wa African Dream mjini Dodoma. Akizungumzia hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali katika mapambano dhidi ya rushwa, alisema Serikali imeanza kupata mrejesho mzuri kwamba watumishi wa umma wanawajibika ipasavyo na vitendo vya rushwa vinaendelea kupungua. “Baadhi ya hatua tulizochukua ni pamoja na kuimarisha taasisi yetu ya TAKUKURU; kuimarisha matumizi ya mashine za kielektroniki ili kupunguza mianya ya kupoteza mapato; kuanzisha mahakama ya mafisadi; kusimamia nidhamu katika utumishi wa um...

Jela Miaka 23 Kwa Kuiba Cheti Kidato cha Nne

Image
Mahakama  ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu kwenda jela miaka 23 mkazi wa kijiji cha Kalovye, Osward Mpalasinge (26). Amepewa adhabu hiyo baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo cheti cha kidato cha nne. Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Teotimus Swai baada ya mshtakiwa kukiri kosa mahakamani. Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Swai alisema mtuhumiwa amekutwa na hatia pasipo shaka hivyo anahukumiwa kwenda jela miaka  23.  Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli alisema mshitakiwa alitenda makosa ya kuvunja na kuiba Mei 25 mwaka huu saa mbili usiku nyumbani kwa Veronica Crispin katika Kijiji cha Kalovye, Inyonga. Alidai kwamba mshitakiwa alifika nyumbani hapo, akavunja na kisha kuiba nguo zenye thamani ya Sh 110,000 na cheti cha kidato cha nne cha Henreth Edward Kalamu, kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) mwaka 2015. Hongoli aliitaka mahakama kutoa adhabu kali kwa mt...

Meya wa Jiji la Arusha Amtaka Mkuu wa Mkoa Amuombe Radhi

Image
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani. "Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma," alisema. Pia, alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu. "Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi...

Breaking News: Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2017

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema kutokana na mwongozo ...