NDOA ZA UTOTONI NI KOSA KISHERIA
| Afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya jiji la Arusha |
Baadhi ya
wakazi wa jiji la arusha na maeneo ya jirani wameombwa kuachana na utaratibu wa
kufuata mila na desturi za zamani za kuwaozesha watoto wao kwa wanaume kabla ya
kufikisha umri wa kuolewa.
Akizungumza
na mwandishi wetu bw.Shija Numbu ambaye ni afisa ustawi wa jamii wa jiji la arusha amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa na
utamaduni wa kuozesha watoto wa kwa ajili ya kujipatia mali na kipato cha
kuendesha maisha yao ya kila siku.
Amesema kuwa
vitendo hivyo vimekuwa vikitokea kila mara hasa kwa mwaka jana na amepokea kesi
mbalimbali za makosa ya ndoa za utotoni ikiwemo ya binti mariamu aliyeozeshwa
na wazazi wake akiwa na umri wa miaka saba.
Aliongeza na
kusema kuwa watoto hao wanapoozeshwa na wazazi wao huenda kulelewa katika ndoa
zao na kufanya majukumu ya kifamilia kama watu wazima jambo ambalo hupelekea
kuwaharibu kisaikolojia.
Bw.shija
ameongeza kuwa watoto hao wamekuwa
wakinyimwa haki zao za kimsingi ikiwemo kukosa elimu,malezi ya wazazi na wakati
mwingine kufanyiwa vitendo vya ukatili kama kukeketwa na hii ni kutokana na utamaduni huo kwa baadhi ya makabila.
Amewaomba
wazazi wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja kwani utu wa mtu
hauwezi ukathamanishwa na kitu chochote pia kwa wale wote wanaofanya vitendo
hivyo wanatakiwa kuheshimu haki za binadamu na watambue kufanya hivo ni kosa
kisheria na yeyote atakayebainika akifanya hivo hatua za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Comments
Post a Comment