YANGA,AZAM KUUVUNJA MWIKO WA WAARABU

WAKATI mechi ya Al Ahly na Yanga itachezeshwa na marefa wa Mali, mchezo wa timu nyingine ya Tanzania katika michuano ya Afrika, Azam FC dhidi ya Esperance utachezewa na marefa wa Morocco.
Marefa wa nchi jirani na Tunisia, Morocco ndiyo watachezesha mechi ya marudiano hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Esperance dhidi ya Azam FC ya Tanzania.
Mechi hiyo itachezwa kesho Uwanja wa Olimpiki Novemba 7 mjini Rades na marefa watakuwa ni Redouane Jiyed atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Mouhib Abdallah Filali na Essam Benbaoa wote wa Morocco.
Marefa wa Mali watachezesha mechi kati ya Al Ahly na Yanga Jumatano mjini Cairo

Azam FC inahitaji kuulinda ushindi wake wa kwenye mchezo wa kwanza wa 2-1 Dar es Salaam ili kusonga mbele katika mchujo wa kuwania kupangwa makundi ya ligi ndogo ya michuano hiyo.
Mechi ya marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika kati wenyeji Ahly na Yanga Uwanja wa Borg el Arab mjini Alexandria, Misri Jumatano utachezeshwa na marefa wa Mali.
Marefa wa Morocco watachezesha mechi kati ya Esperance na Azam kesho

Hao ni Mahamadou Keita atakayepuliza kipyenga akisaidiwa na Balla Diarra na Drissa Kamory Niare, wote wa Mali.
Yanga inahitaji ushindi wa ugenini Jumatano ili kwenda hatua ya makundi ya michuano hiyo, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam. 
Iwapo Yanga itatolewa, itakwenda kumenyana na moja ya timu nane zilizofuzu kwenye Kombe la Shirikisho kuwania kupangwa kwenye makundi ya kucheza michuano hiyo ya pili kwa ukubwa ya CAF katika ngazi ya klabu.

CHANZO:BIN ZUBERY

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA