Mama Janeth Magufuli aahidi kuendelea kusaidia kambi za wazee na watu wenye ulemavu nchini.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli ameahidi kundelea kusaidia kambi za wazee na watu wenye ulemavu ikiwamo ukoma kutokana na kundi hilo kusahaulika kwa muda mrefu.
Mama Janeth ameyasema hayo wakati wa hafla ya utoaji wa Msaada wa vyakula, Mafuta kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi pamoja na madawa katika kambi ya wazee na watu wenye ulemavu ya Nandanga iliyopo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Aidha Mama Janeth Magufuli amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kundi hilo mpaka sasa kwa kushirikiana na wadau wengine ameshatoa Misaada katika Kambi 4 za Mikoa ya Dar es Salaam (NUNGE) Mwanza (BUKUMBI), Lindi (NANDANGA) na Mtwara (NKASEKA) ambayo inathamani ya takribani shilini Milioni 250.
Katika hatua nyingine Mama Janeth Magufuli alizindua jiwe la msingi kwenye Jengo la Zahanati Zahanati ya Nandanga itakayorahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Naye Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa amemshukuru Mama Janeth kwa uamuzi wa kutembelea kambi hiyo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kumuunga mkono ili kusaidia watu wenye ulemavu na wazee.
Akiongea kwa Niaba ya Wazee wa Kambi ya Nandanga Mratibu wa Kambi hiyo Bw. Agnerus Chiamba alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa Misaada hiyo kwani itawasadia kwa kiasi kikubwa kutokana na uhitaji waliokuwa nao.
Comments
Post a Comment