MKENYA ATWAA TUZO YA MAZINGIRA MAREKANI

Mwanamazingira wa Kenya Tom Lalampaa ameshinda tuzo ya mazingira kutokana na juhudi zake kwenye kurudisha ardhi iliyoharibiwa Kaskazini mwa Kenya.

Tom Lalampaa

Lalampaa amekuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hiyo ya Bright inayotolewa kila mwaka na Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani, kwa watu wanaoonyesha rekodi nzuri ya ulinzi wa mazingira. Lalampaa pia anapewa tuzo hiyo kutokana na kuhimiza masikilizano ya kijamii na kulinda mazingira ya asili.

Tom Lalampaa

Kwa sasa Lalampaa ni Mkuu wa Mfuko wa Northern Rangeland, ambao unahamasisha jamii za wafugaji kuwa sehemu ya mbinu za kisasa za uhifadhi wa mazingira, zinazohusisha wanyamapori, watu na mazingira ya asili.

Comments

Popular posts from this blog

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA

DC AWAAGIZA WALIOVAMIA EPZA WAONDOKE.

Je Umewahi Kujiuliza Mwezi nusu Kwenye Kucha yako Una Maana Gani? Jibu lake ni Muhimu Kuliko Unavyofikiria!