UTANDO WA BUIBUI SAWA NA ALMASI ILIYO MCHANGANI

Wahenga walisema penye miti hapana wajenzi na asiyejua maana haambiwi maana! Leo navunja sheria kwa kukwambia juu ya thamani ya utando wa buibui ambao wengi wetu huuona na kuupuuzia pasipo kujua kazi yake kwa kudhani ni uchafu usio na faida yoyote.

Utafiti mpya ulioripotiwa na Gazeti la Nano Letters la Marekani unaonesha kuwa utando wa buibui ni malighafi nzuri ya kimaumbile ya kutengeneza darubini, na inaweza kutumiwa kuinua uwezo wa darubini za jadi za kuangalia vitu vidogovidogo viilivyotengenezwa kwa vioo.

                        utando wa buibui

Kama bado ulikuwa hujaipata hiyo sasa ufahamu na kutilia maanani utafiti ulioongozwa na Dk. Wang Zengbo kutoka Chuo Kikuu cha Bangor cha Uingereza kwa kushirikiana na Prof. Fritz Vollrath kutoka Chuo Kikuu cha Oxford.

Kutengeneza darubini kwa utando wa buibui ni rahisi sana. Watafiti waliweka utando wa buibui juu ya kitu kitakachoangaliwa, kutia kileo katika kitu hicho na utando wa buibui, halafu kuangalia kitu hiki kupitia darubini ya kawaida ya vioo. Utando wa buibui unainua uwezo wa darubini ya vioo kwa mara mbili hadi tatu, na kuwawezesha kuona vitu vidogovidogo vyenye urefu wa nanomita 100 tu. Wakitumia darubini ya vioo tu hawawezi kuona.

bui-bui

Dk. Wang amesema aligundua jambo hili kwa bahati. Siku moja alipocheza na mtoto wake katika ua wa nyumba yake aliona utando wa buibui. Ghafla akapata wazo la kutengeneza darubini kwa utando huo, baadaye alithibitisha kuwa wazo hili kweli linafanya kazi.

Comments

Popular posts from this blog

ZINGATIA HAYA UKITAKA KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

Waziri Mkuu Ashangazwa Na Kodi Kubwa Soko La Dodoma.....Aagiza Baraza La Madiwani Lipitie Upya Na Kumpa Majibu

ALAMA YA NYOKA KWENYE NEMBO MBALIMBALI INA MAANA KUBWA