Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana bado yanaiumiza Chadema ambayo imesema haitakubali yaliyotokea yajirudie katika uchaguzi ujao. Katika uchaguzi huo, chama hicho kilishika nafasi ya pili nyuma ya CCM lakini kililalamikia matokeo huku kikisema kulikuwa na ukiukwaji wa taratibu na sheria za uchaguzi. Rais John Magufuli alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura 8,882,935, huku mpinzani wake, Edward Lowassa wa Chadema akipata kura 6,072,848. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji amesema chama hicho hakitakubali kudhulumiwa kwa namna yoyote ile ushindi “Hii inaonyesha katika nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki. Wewe umefanya mara ya kwanza, tukanyamaza, ukafanya tena mara ya pili tena kwa ubabe, tukalalamika, badala ya kusema njooni tuongee, unasema nendeni kokote. Sawa, tusubiri awamu ya tatu. Tukishindwa tutakupongeza, lakini tukishinda shughuli yake itakuwa ngumu,” amesema. Kuhusu utawala wa Rais Magufuli, Dk Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji wa utawala