Nyoka anatumika kwa sababu ya maisha halisi ya mnyama huyu ambaye baada ya muda katika maisha yake huwa anavua gamba na kuota tena kuwa kitu kipya; maana yake ni maisha mazuri, maumivu wakati wa kuvua gamba na uponyaji wakati anapoendelea na maisha ya baadaye. Kwenye huduma za matibabu na baadhi ya majeshi utaona fimbo iliyozungukwa na nyoka, utaweza kuikuta kwenye hospitali karibu zote, huduma zote za afya na sehemu nyingine nyingi fimbo hii ni alama ya Kigiriki iliyotumika kwa maelfu ya miaka inaitwa Rod of Asclepius au Staff of Asclepius. Ni fimbo ya Mungu wa Kigiriki anayeitwa Asclepius anayehusishwa na mambo ya uponyaji na matibabu. Aesculapia ni nyoka waliokuwa wanatumika katika mahekalu ya kutolea matibabu, nyoka hawa walikuwa huru katika vyumba vya wagonjwa waliokuwa wamelazwa ndani toka mwaka 300. Lakini kwa tamaduni za Wahindu suala hili limeenda mbali zaidi katika kueleza mfumo wa vyakula, maisha, matibabu ya asili na mengine mengi. Sehemu kama Thailand nyoka...
Comments
Post a Comment