
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amesema halmashauri yake haitasita kuvunja mikataba ya kampuni za maegesho zinazokiuka matakwa ya mikataba ya Jiji.
Mwita ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya kero zinzodaiwa kufanywa na mawakala hao wakiwa katika majukumu yao huku akitolea ufafanuzi suala la upandishwaji wa ushuru wa maegesho ya magari pamoja na kampuni zinazokamata magari kinyume cha sheria.
“Kampuni za maegesho zikumbuke wajibu wake kisheria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mawakala wake wanafanyakazi bila ya kuwasumbua wananchi kwa lengo la kujipatia fedha,” amesema.
Kuhusu ukamatwaji wa vyombo vya usafiri holela na mawakala wa kampuni za maegesho, Mwita ametoa maagizo kwamba mawakala hao wasikamate magari yaliyowekwa katika sehemu isiyo rasmi hadi ipite dakika 60.
Mwita ameongeza kuwa atafanya ukaguzi juu ya utekelezaji wa maagizo hayo ifikapo january Mosi mwakani nakuwataka wananchi kuwa makini kwawatu ambao wanatoa Huduma ya maegesho pasikuwa na risiti.
Amesisitiza endapo mtoa huduma atabainika anatoa huduma ya maegesho pasipokuwa na risiti pamoja na Efd mtoa huduma hiyo atafikishwa katika vyombo vya sheria nakufutiwa leseni yausajili.
Comments
Post a Comment