Posts

NDOA ZA UTOTONI NI KOSA KISHERIA

Image
Afisa ustawi wa jamii wa halmashauri ya jiji la Arusha Baadhi ya wakazi wa jiji la arusha na maeneo ya jirani wameombwa kuachana na utaratibu wa kufuata mila na desturi za zamani za kuwaozesha watoto wao kwa wanaume kabla ya kufikisha umri wa kuolewa. Akizungumza na mwandishi wetu bw.Shija Numbu ambaye ni afisa ustawi wa jamii wa  jiji la arusha  amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa na utamaduni wa kuozesha watoto wa kwa ajili ya kujipatia mali na kipato cha kuendesha maisha yao ya kila siku. Amesema kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikitokea kila mara hasa kwa mwaka jana na amepokea kesi mbalimbali za makosa ya ndoa za utotoni ikiwemo ya binti mariamu aliyeozeshwa na wazazi wake akiwa na umri wa miaka saba. Aliongeza na kusema kuwa watoto hao wanapoozeshwa na wazazi wao huenda kulelewa katika ndoa zao na kufanya majukumu ya kifamilia kama watu wazima jambo ambalo hupelekea kuwaharibu kisaikolojia. Bw.shija ameongeza kuwa  watoto hao wamekuwa wakinyi...

Gharama za umeme kushushwa

Image
 Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Felichesmi Mramba SHIRIKA la Umeme (Tanesco) limewasilisha katika Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) maombi ya kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 pamoja na kuondoa kabisa gharama za maombi ya awali ya wateja wapya na gharama za huduma kwa wateja wa majumbani. Gharama za maombi hayo ya awali ambayo pia yanajulikana kama gharama za fomu ni Sh 5,900 na gharama za huduma (service charges) ni Sh 5,520 kwa mwezi kwa wateja wa majumbani. Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanseco,  Felichesmi Mramba alisema kuwa kisheria maombi hayo yanatakiwa kujibiwa ndani ya siku 24 ambapo wanaamini kuwa watapata majibu mazuri. Mramba alisema gharama za huduma zimekuwa zikiathiri sana watumiaji wa umeme wa majumbani tofauti na wanaotumia viwandani. Mramba alisema kuwa maombi hayo yamewasilishwa baada ya Tanesco kufanya tathimini ya kina kimahesabu pamoja na kubuni namna ambayo wateja wao w...

TPB YATOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA SACCOS KIGOMA, NI MPANGO WA KUINUA MITAJI YA WAJASIRIAMALI.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa  Machibya, (kushoto), akimpatia mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 75 Kaimu mwenyekiti wa Saccos ya Ishimwe Kigoma Bi.Gabriela Hangula wakati wa  hafla ya kukabidhi fedha kwa vikudi vya benki za vijijini (VICOBA), mkoani humo,.  Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma. John Ndungulu, Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania, (NEEC), Bi. Beng’ Issa na Afisa Mtendaji Mkuu, (CEO) wa Benki ya Posta Tanzania, Bw. Sabasaba Moshingi.Benki ya Posta imekabidhi jumla ya silingi milioni 175 kwa vikundi hivyo viwili ikiwa ni mpango wa kuwawezesha wananchi kwa kuwakooesha fedha kuinua mitaji yao chini ya udhamini wa baraza hilo.  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya (kushoto), akimpa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Saccos ya TWCC Kigoma, Dorothy Takwa. Wa pili kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Jo...

Mashambulizi mapya Syria kuchunguzwa

Image
Image caption Usitishwaji wa mapigano umefanikisha shughuli za binadamu Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry amesema madai yote ya kuvunja muafaka wa kusitisha mashambulizi nchini Syria yatachunguzwa. Hata hivyo Kerry amesisitiza kwamba Marekani na Urusi wameafikiana kutojadili madai hayo hadharani. Image caption Watoto wameanza kucheza baada ya mashambulio kusimama Ameongeza pande hizo zimekubaliana kuhakikisha mashambulizi yanalenga ngome za wapiganaji wa Islamic State na Al-Nusra Front pekee. Makundi hayo hayajawekwa kwenye muafaka wa kusitisha mapigani kwa muda ili kuwezesha shughuli ya kusambaza misaada ya kibinadamu nchini Syria.

Kigogo wa Republican amkataa Trump

Image
Image copyright Getty Image caption Trump ametuhumiwa kwa kuwagawanya Wamarekani Seneta wa Nebraska Ben Sasse amesema hatamuunga mkono mgombea urais anayengoza miongoni mwa wagombea wa chama cha Republican Donald Trump. Sasse ndiye mwachama wa kwanza wa ngazi ya juu wa chama cha Republican aliyechaguliwa kutangaza hadharani kwamba hatamuunga mkono Trump. Amesema amesikitishwa sana na kuvunjwa moyo na mfanyabiashara huyo na kwamba atamtafuta mgombea mwingine wa kumuunga mkono iwapo Trump atashinda uteuzi wa Republican. Bw Trump tayari ameshinda uchaguzi wa mchujo katika majimbo matatu kati ya manne yaliyofanya mchujo kufikia sasa. Aidha, anaongoza kwenye kura za maoni katika majimbo 11 ambayo yatapiga kura ya mchujo Jumanne. Uchaguzi wa leo wa mchujo ambao hufanya siku hii kujulikana kama “Jumanne Kuu” huwa muhimu sana kwa wagombea kwani huamua wale walio na nafasi ya kushinda na wale wasio na uwezekano wa kushinda. "Iwapo Donald Trump atakuwa mgombea wa Republican, ni...

Mbowe Apinga Watumishi wa Umma Kutumbuliwa MAJIPU Bila Kupewa Nafasi ya Kusikilizwa Kwanza

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amepingana  na  sera  ya  Rais John Magufuli  ya kuwatumbua majipu watumishi wa umma wazembe na wabadhilifu wa mali za umma. Mbowe amedai kuwa Serikali Magufuli imekuwa ikiwatimua watumishi mbalimbali wa umma bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza kupitia kampeni ya kupambana na ufisadi, inayotambulishwa kwa kaulimbiu ya ‘utumbuaji majipu’. Akizungumza jana katika ibada maalumu ya shukrani kwa kumaliza uchaguzi mkuu salama, iliyofanyika kwenye Usharika wa Nshara wa Dayosisi ya Kaskazini ya KKKT na kuhudhuriwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Frederick Shoo, na maaskofu wastaafu Dk. Erasto Kweka na Dk. Martin Shao, Mbowe alisema (wapinzani) hawaridhishwi na hatua ya serikali ya Rais Magufuli kuendeleza timuatimua na kuwasimamisha kazi watumishi wa umma 160 tangu aingie madarakani bila kuwapa nafasi ya kuwasikiliza. Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, a...

Halmashauri Ya Jiji la Tanza Hatarini Kufutwa

Image
Wakati sakata la kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam likiendelea kupamba moto baada ya mchakato huo kuwekewa zuio la mahakama juzi, serikali imetishia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Tanga iwapo haitamaliza mgogoro wake wa kisiasa. Akizungumza na viongozi serikali na kisiasa jijini Tanga jana, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, alisema serikali italazimika kuivunja halmashauri hiyo endapo mgogoro huo hautamalizwa haraka, kutokana na ukweli kwamba tangu kuanza kwa uongozi wa awamu ya tano baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana imeshindwa kufanya vikao vyake halali kwa mujibu wa katiba kutokana na mgogoro wa kisisa bina ya Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa, huku wananchi wakishindwa kutatuliwa kero zao kwa wakati hivyo kuzorotesha maendeleo yao. “Mpaka sasa jiji la Tanga hakuna uongozi uliosimama, sasa hatuwezi kwenda kwa mwendo huu, wananchi wanahitaji maendeleo na kurudia uchaguzi hatuwezi ni gharama kubwa, kilichobaki ni kuivunja ha...