Posts

Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9

Image
Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2015. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli  hizo zimekuwa  kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Kwa upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua  na ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto. Aidha shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 20...

MKENYA ATWAA TUZO YA MAZINGIRA MAREKANI

Image
Mwanamazingira wa Kenya Tom Lalampaa ameshinda tuzo ya mazingira kutokana na juhudi zake kwenye kurudisha ardhi iliyoharibiwa Kaskazini mwa Kenya. Lalampaa amekuwa mwafrika wa kwanza kupata tuzo hiyo ya Bright inayotolewa kila mwaka na Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani, kwa watu wanaoonyesha rekodi nzuri ya ulinzi wa mazingira. Lalampaa pia anapewa tuzo hiyo kutokana na kuhimiza masikilizano ya kijamii na kulinda mazingira ya asili. Kwa sasa Lalampaa ni Mkuu wa Mfuko wa Northern Rangeland, ambao unahamasisha jamii za wafugaji kuwa sehemu ya mbinu za kisasa za uhifadhi wa mazingira, zinazohusisha wanyamapori, watu na mazingira ya asili.

TUNZA SIRI ZA MUMEO HASA ZA FARAGHA

Image
Mahaba leo itawaangazia wale wote ambao wakipewa chakula harakaharaka kesho yake kukimbilia kwa jirani na kumsimulia, utasikia; “leo baby wangu amenilisha vijiko vingi hadi nimechoka! Ni fundi wa kulisha kweli tena kwa mikono yote” sasa unamwambia ili iweje, ina husu? Umeshamuamsha mwenzako, akaamka na kuhamasika sasa akimtamani na yeye akapewa hicho chakula na mumeo utamlaumu nani? Wengine wanafika mbali na kusimulia udhaifu wa mumewe utasikia; “Yaani shoga, mume wangu hakuwa hivi, siku hizi anarudi amechoka kweli, ananipa kijiko kimoja tu anadai amechoka” sawa amechoka, wa kukusaidia kujua kwa nini amechoka ni jirani kweli? Jifunze kutunza siri ya chakula chako na mumeo. Iwe anakulisha kwa mikono yote, iwe anashindwa kukulisha hiyo ni siri yako na yeye. Wengine wao wakikaa kama kusukana au gengeni ama kwenye makundi ya Mtandao wa WhatsApp stori zao kubwa ni kila mmoja kumuelezea mumewe utasikia; ‘Leo usiku sijalala, nimemuandalia vyakula vyote, kala akaniambia hajashiba, ...

Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)

Image
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, atatua ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam Maalim anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi. Hatua ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho. Azma yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na genge la wafuasi wake. Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11 baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la Taifa (BKT), lililokutana Visiwani. ...

JINSI YA KUTENGENEZA BWAWA LA KUFUGIA SAMAKI?

Image
Zipo namna mbalimbali za utengenezaji wa bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa lenyewe. Aina ya bwawa la kufugia samaki. Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea "Earthen Pond" ambalo litakuwepo mahali ambapo udongo unaruhusu kutuwamisha maji. Mara nyingi kuta zake hushindiliwa na kupandwa nyasi ili kupunguza nguvu ya maji kasababisha mmomonyoko wa udongo.  Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea "Earthen Pond" ambalo litakuwepo mahali ambapo udongo hauruhusu kutuwamisha maji, litatandikwa Karatasi la "Nylon"/"Polythene sheet" ili kuzuia maji yasipotee ardhini.     Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa Matofali, Cementi na Zege; Kwenda chini ya ardhi "Earthern concrete pond" Kwenda juu ya ardhi "Raised Conrete Pond" 

Utafiti Twaweza: Nchi Haiongozwi Kidikteta...!!

Image
Asilimia 58 ya Watanzania wamepinga kauli za baadhi ya wanasiasa kuwa Rais John Magufuli anaendesha nchi kidikteta huku asilimia 31 imesema haina uhakika na jambo hilo. Aidha, imeelezwa kuwa asilimia 80 ya wananchi wanaona kwamba baada ya uchaguzi juhudi za kimaendeleo zipewe kipaumbele na vyama vya siasa. Akitoa taarifa za utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Twaweza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Aidan Eyakuze alisema ni asilimia 11 pekee ya Watanzania ndiyo waliosema nchi hii inaongozwa kidikteta. “Baadhi ya wanasiasa na wasomi walitafsiri uongozi wa Rais Magufuli kama udikteta na neno hilo likawa mojawapo ya mambo yaliyounda Ukuta, asilimia 11 wanakubaliana na wazo hilo lakini asilimia 58 wanalipinga huku asilimia 31 wanasema hawana uhakika,”  alisema Eyakuze. Alisema kundi kubwa ambalo limejibu kuwa Rais Magufuli ni dikteta ni la vijana na watu matajiri na wenye uwezo wa juu kiuchumi kuliko masikini, wazee na watu wenye elimu...

MWANASIASA WA UPINZANI AKAMATWA KUSINI MWA BURUNDI

Image
Bujumbura, Februari 3, 2016. Burundi, mzunguko wa vurugu na ukandamizaji vinandelea kushuhudiwa kwa mwaka mmoja sasa. Nchini Burundi duru za usalam zinaarifu kwamba mwanasiasa wa upinzani nchini humo Gervais Niyongabo alikamatwa Jumatano kwa kosa la "kuhatarisha usalama wa taifa". Bw Niyongabo alikamatwa mkoani Makamba, kusini mwa Burundi. Kwa mujibu wa msemaji wa polisi ya Burundi, Pierre Nkurikiye, mwanasiasa huyo kwa sasa anazuiliwa mjini Bujumbura na Idara ya Ujasusi (SNR), ambayo ni iko moja kwa moja chini ya mamlaka ya Rais Pierre Nkurunziza. Idara ya Ujasusi ya Burundi inatuhumiwa na mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu kutujihusisha na mateso dhidi ya wapinzani. Wafuasi wengi kutoka upinzani nchini Burundi wameitoroka nchi hiyo kufuatia machafuko yaliyoikuba tangu mwezi Aprili 2015. Machafuko hayo yalizuka kufuatia uamuzi wa Pierre Nkurunziza wa kuwania muhula mwingine katika uchaguzi wa irais uliyofanyika mwezi Julai 2015, baada kuchaguliwa kwa m...