Posts

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI DEC 22,HABARI KUU ZIJUE KAULI TANO ZA JPM ZILIZOTIKISA 2016

Image

Rais wa Gambia: Hakuna wa kunitoa Madarakani, labda Mungu Pekee

Image
Rais wa Gambia Yahya Jammeh amesema kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa eneo la magharibi mwa Afrika la kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mpinzani wake, Adama Barrow. Akihutubia Wanachama wa Muungano nchini humo Bw. Jammeh amesema: ”Waje wajaribu kuniondoa wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi”. “Mimi sio muasi, haki yangu haiwezi kuvurugwa. Hii ni nafasi yangu, hakuna mtu anayeweza kuniondoa labda Mungu,” amesema. Amesema kuwa alikataa wito wa Muungano wa Viongozi wa Mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia. “’Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu,” amesema na kuwashutumu viongozi hao kwa kuingilia mambo ya ndani ya Gambia. ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua Bw. Barrow kama Rais wa taifa hilo na kwamba litachukua...

IDADI YA WATU WALIOFARIKI BAADA YA KUNYWA SABUNI WAKIDHANIA NI POMBE YAONGEZEKA

Image
Idadi ya watu waliofariki baada ya kunywa sabuni wakidhania ni pombe imefikia watu 58 kutoka 49 kulingana na vyombo vya habari nchini Urusi, Wengi wa watu 37 walioathirika bado wanaendelea kutibiwa huku wengine wakiwa katika hali mahututi. Raia hao walikunywa maji ya sabuni yaliokuwa na sumu kali wakidhania ilikuwa pombe kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi,lakini maji hayo yalikuwa na kemikali ya Ethanol inayoweza kusababisha upofu.

RAIS MAGUFULI AKATAA SHULE KUITWA JINA LAKE

Image
Rais John Magufuli amekataa shule ya msingi iliyojengwa hivi karibuni eneo la Bunju, Wilaya ya Kinondoni kuitwa kwa jina lake badala yake ameagiza iitwe kwa jina la Mkuu wa wilaya hiyo, Ally Hapi.  Taarifa ya badiliko la jina haikutolewa na Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kama ilivyozoeleka bali na mkuu wa wilaya hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa uongozi wa shule hiyo.  “Shule hii imejengwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi.  Shule hiyo mpya iliyopo Bunju jijini imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Bunju A ambayo ilikuwa na wanafunzi 3,224. Mwalimu mkuu wa shule hiyo mpya, Ali Mwakapalila alisema ingawa inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwakani inakabiliwa na changamoto mbalimbali.  “Hak...

Polisi yamnasa mtuhumiwa Sugu wa utapeli Tanzania

Image
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa  kumkamata mtuhumiwa wa utapeli anayejulikana kwa jina la  Wilfred Masawe (36) ,  mkazi wa  Buza, Temeke jijini Dar es Salaam. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi Mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu mbalimbali kutapeli zikiwemo kujitambulisha kama kiongozi wa serikali kwa kutumia mtandao wa Whatsapp,  huku akieleza kuwa yupo nje ya nchi na kuna tatizo la msiba ambao umetokea nchini na unamuhusu na hivyo alikua akitoa maelekezo kwa watendaji wa serikali waweze kusaidia gharama za matibabu hospitalini, gharama za kusafirisha mwili wa marehemu na gharama za mazishi. Taarifa hiyo pia imesema mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia mbinu ya kujifanya kiongozi mkubwa wa dini ya kikristo (Askofu) na kuwaambia waumini na viongozi mbalimbali kuhusu maandalizi ya makongamano ya kidini kwa lengo la kuwaomba michango kuweza kufanikisha makongamano hayo. Baadhi ya matukio aliyofanikiwa kutapeli ni pamoja na kuwata...

JAMII YATAKIWA KUHESHIMU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU - DKT. POSSI

Image
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Dkt. Abdallah Possi ameitaka jamii kuzingatia haki na usawa kwa watu wenye ulemavu nakuondokana na imani potofu za kuona watu wenye ulemavu hawana uwezo wa kufanya shughuli za maendeleo. Mhe. Possi ameyasema hayo kwa nyakati tofauti alipotembelea Vituo na Shule zinazohudumia watu wenye mahitaji maalum vya Nandanga, Rasi Bula, Shule ya msingi Nyangao mkoani Lindi pamoja na makazi ya wenye ulemavu na Ukoma ya Mkaseka, Chuo cha wenye Ulemavu cha Mtapika, shule ya Lulindi na Masasi mkoani Mtwara. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe. Dkt. Abdallah Possi akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika shule ya Masasi yenye kuhudumia wenye ulemavu Mkoani Mtwara. Katika ziara hiyo Mhe.Possi alisisitiza jamii zibadili mitazamo hasi juu ya masuala ya haki na usawa kwa watu wenye ulemavu kwa kuwashirikisha katika ...

HARUFU YA MAITI SABA MTO RUVU YAFANYIWA KAZI

Image
Siku moja baada ya magazeti  kuripoti taarifa za kuwapo harufu mbaya na majimaji yanayotoka ilipozikwa miili ya watu saba waliofungwa kwenye viroba, Bibi Afya wa Wilaya ya Bagamoyo, Joyce Nganzo ametembelea eneo hilo kuona hali halisi. Desemba 8, mwaka huu maiti saba ziliokotwa katika Mto Ruvu na muda mfupi baadaye zilizikwa kando ya mto huo huku Serikali ikiahidi kuendelea na uchunguzi. Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Nganzo alisema atakabidhi taarifa ya alichokiona kwa mkurugenzi wa halmashauri ya Bagamoyo kwa ajili ya kuifanyia kazi. “Nilikwenda, taarifa nitampa Mkurugenzi, yeye ndiyo atakuwa na maamuzi zaidi,” alisema Nganzo. Katibu wa Kitongoji cha Mtoni, kata ya Makurunge, Mukhtari Shebule alisema, “Tunashukuru mmeliweka wazi suala hili, bibi afya alikuja kuangalia hali halisi, tunasubiri hatua zitakazochukuliwa kunusuru afya zetu,” alisema Shebule. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Hemed Mwanga alisema hana cha kuzungumza na baada ya kukamilika uchunguzi watatoa taarifa....