Posts

Meya wa Jiji la Arusha Amtaka Mkuu wa Mkoa Amuombe Radhi

Image
Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametoa siku saba kwa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amuombe radhi kwa kosa la kumuweka ndani wakati alipokuwa anakabidhi rambirambi kwa wazazi waliofiwa kwenye ajali ya gari la Shule ya Msingi Lucky Vincent. Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Ijumaa, Lazaro alisema mpaka sasa ameshindwa kuelewa ni kwanini mkuu huyo aliagiza meya pamoja na wenzake wakiwemo viongozi wa dini, madiwani, wawakilishi waliotoa rambirambi na mwenye shule kukamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani. "Mimi sikuwa na shida na RC na kitendo cha kumuweka ndani kiongozi wa dini, paroko, kiongozi wa dini ya Kiislamu ni kitendo ambacho si cha kibinadamu na anapaswa aombe radhi umma," alisema. Pia, alimtaka kutafakari nafasi yake na kuona kuwa anafaa kuendelea kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha kwasababu ameonyesha kuwatumikia wananchi ambao hawaheshimu. "Hana heshima na mbunge, madiwani, watu wenye degree zao, haheshimu viongozi...

Breaking News: Orodha ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Tano na Vyuo Vya Ufundi 2017

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) George Simbachawene ametoa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya ufundi kwa mwaka 2017 huku jumla ya wanafunzi 2,999 wakiachwa. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akizungumza na waandishi ws habari na kusema kuwa ufaulu kwa mwaka huu umeongezeka kwa asilimia 3.75 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2015. Waziri amedai kati ya wanafunzi 96,018 waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni wanafunzi 93,019 tu ndiyo waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. Waziri Simbachawene amesema kuwa jumla ya watahiniwa wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne kwa shule kwa mwaka 2016 ni 349,524 huku waliofanya mtihani wa kujitegemea ni 47,751 ambapo watahiniwa waliofanya mtihani wa shule waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani Tanzania Bara. Simbachawene alisema kutokana na mwongozo ...

IGP Sirro afanya ziara Kibiti na Rufiji.....Atangaza msako mkali

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro  jana alifanya mazungumzo na wazee pamoja na viongozi wa dini wilayani Kibiti mkoani Pwani ili kubaini waalifu wanaotekeleza mauaji ya watu wilayani humo na kusema vyovyote itakavyokuwa lazima watawarudisha kwenye msitari. IGP Sirro alisema kupitia mazungumzo hayo tayari amepata taarifa za wahalifu hao ingawa ni mapema kuziweka wazi ila amewakikishia wananchi kuwa waalifu wao ni lazima watapatikana. “Kubwa ni kwamba wazee wetu wa Kibiti wametueleza taarifa nyingi sana na mnavyojua hawa waalifu wanaishi ndani ya Kibiti, ndani ya Ikwiriri, kwa hiyo wazee wetu wamejaribu kutueleza ni wapi tunaweza kuwapata na chanzo cha mambo yote haya,”  alisema IGP Sirro na kuongeza; “Kwa hiyo kimsingi mambo mengine mengi ni ya kipelelezi ambayo siwezi kuyasema kwa sasa, lakini kikubwa wametupa dira, muelekeo kwa maana kwamba wale ndugu zetu au maadui zetu kwa lugha nyepesi tumepata njia nzuri ya kudeal nao. Kwa hiyo nitume salamu...

Halima Mdee na Ester Bulaya Kulipwa nusu mshahara kwa miezi 10 nje ya Bunge

Image
Wabunge wa Chadema, Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini) ambao wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge, watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi kumi. Stahiki hizo ni kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya Bunge inayosema, “mbunge aliyesimamishwa hataingia tena sehemu yoyote ya ukumbi na maeneo ya Bunge kwa muda wote atakapokuwa amesimamishwa na atalipwa nusu mshahara na nusu posho zinazoambatana na mshahara huo.” Vilevile, kutokana na uamuzi huo wabunge hao watakosa siku 65 za Bunge zinazojumuisha siku 25 zilizobaki za Bunge la bajeti linaloendelea, Bunge la Oktoba na lile la Februari, 2018. Vikao vya mabunge hayo mawili; la Oktoba na Februari kila kimoja huwa na mikutano ya wiki mbili mbili. Wabunge hao walisimamishwa juzi kwa azimio la Bunge licha ya kutokuwapo au kujitetea kutokana na tuhuma zilizokuwa zinawakabili za kudharau kiti cha spika. “Tukutane Bunge lijalo la bajeti,” alisema juzi Spika wa Bunge, Job Ndugai. Bunge la bajeti huan...

Rose Muhando Atiwa Mbaroni mkoani Singida kwa Utapeli

Image
Jeshi  la Polisi Mkoa wa Singida linamshikilia mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili, Rose Muhando akituhumiwa kujipati fedha kwa njia ya udanganyifu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Debora Mgiligimba alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mwimbaji huyo alikamatwa juzi Wilaya ya Ikungi baada ya wadeni wake ambao ni Waumini wa Kanisa la AICT Singida kupata taarifa kuwa yupo wilayani humo. Inadaiwa kuwa Novemba 3 mwaka jana, mwimbaji huyo alitumiwa fedha na Mwenyekiti wa Kwaya ya Kanisa la AICT Singida, Mashala Japhet Tsh 800,000 ambapo zilitumwa baada ya pande mbili kukubaliana kuwa angekwenda kwenye uzinduzi wa Album ya kwaya na kanisa hilo, hata hivyo hakutokea. Kwa mujibu wa kamanda huyo, uzinduzi wa kwaya hiyo ulikuwa ufanyike Novemba 13 mwaka jana, saa 8 mchana katika uwanja wa Namfua Singida. Novemba 8 mwaka jana, mwimbaji huyo aliomba kutumiwa tena 150,000 kwa ajili ya nauli ya kutoka Dodoma kwenda Sing...

Lowassa, Sumaye, Mabata Watema Cheche Msibani

Image
Viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki ya kisiasa.  Katika hatua nyingine, wameshangazwa na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alisema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia.  “Nawapongeza kwa maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure." Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Pwani, Fredrick Sumaye alisema “ Hata njia za kupitisha maiti nazo zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu  ya amani aliyoipanda Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.” ...

Ally Kessy: Wabunge Wanaotusumbua Bungeni Wapimwe Madawa ya Kulevya

Image
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy amependekeza kuwapo na sheria ya kuwapima wabunge matumizi ya dawa za kulevya ili kuepukana na ukorofi unaojitokeza bungeni mara kwa mara. Keissy alisema hayo jana bungeni mjini Dodoma na kusisitiza kuwa yeye atakuwa mstari wa mble kwenye upimaji na endapo itatokea mbunge yoyote yule atakayebisha kupimwa kipimo hicho basi apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge. "Tutengeneze sheria sisi sote hapa tupimwe, inawezekana kuna watu wanatumia madawa ya kulevya humu, tena mimi nitakuwa wa kwanza, tupimwe kuondoa tatizo kwenye bunge letu hili la ukorofi na atakayekataa apimwe kwa nguvu na afukuzwe ubunge haiwezekani kurudia makosa mtu mmoja kila siku anasemwa anarudia yale yale"  alisema Keissy na kuongeza; "Adhabu ndogo hii lazima ziwe kali wasipate chochote, wasionekane bungeni muda wa miezi sita au saba ndiyo watashika nidhamu katika bunge hili. Haiwezekani tunaonekana kama tupo Manzese, wabunge wa mjini wamezoea kwenye ...